Kwa mujibu wa Wafanyabiashara hao, taarifa za kuondoka katika eneo hilo zimewafikia asubuhi, huku zoezi la ubomoaji likianza muda wa mchana.
Wafanyabiashara hao wamedai zoezi hilo limekuwa la ghafla kwani hawajapewa muda wa kutosha kuhamisha bidhaa zao huku wakishuhudia meza zao zikibomolewa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa soko hilo, amesema pamoja na kuwa amewahi kuwataangazia Wafanyabiashara kuahusu ujio wa suala hilo, lakini taarifa rasmi ameipokea asubuhi huku zoezi likianza kuendeshwa mchana.
Naye afisa biashara wa halmashauri ya wilaya ya Ilemela amesema waliobomolewa meza , ni wale waliozitelekeza kwa muda mrefu huku baadhi yao wakijimilikisha maeneo ya halmashauri hiyo.