
Kupitia kampeni ya Namthamini, leo timu ya East Africa Television LTD imeweka kambi pale City Mall jijini Dar es salaam huku wasanii na wadau mbalimbali wakijitokeza kushiriki kuchangia upatikani wa taulo za kike (Pads).
(Meneja wa Maisha Super Market Emodia Lyoid)
Moja ya wadau ambao wamejitokeza pia ni Maisha Super Market ambao maduka yao yapo ndani ya jengo la Citty Mall. Meneja wa Super Makert hiyo Emodia Loyd amepongeza kampeni hiyo na kueleza kuwa jambo hilo linatakiwa kufanyika mara kwa mara.
"Sisi kama Maisha Super Market ambao tuko hapa City Mall tumeamua kutoa pakiti zaidi ya 600 kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike hasa waliopo shuleni naomba EATV na EARadio kwa jambo hili kubwa tuweze kufanya mara kwa mara." amesema Loyd.
Kampeni ya Namthamini inayoondeshwa na EATV na EARadio inalenga kuwanusuru wanafunzi wa kike.