Jumatatu , 18th Jul , 2022

Wadau wa utalii hususani wakala wa biashara za utalii, watoa huduma za malazi, wakala wa safari na waongoza watalii wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zitakazotokana na onesho la Swahili International Tourism Expo (S!TE) litakalofanyika Dar es Salaam Oktoba 21 hadi 23, 2022.

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Balozi Dkt. Pindi Chana.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Balozi Dkt. Pindi Chana Jijini Arusha alipokua akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu onesho hilo la sita, litakalofanyika, Jijini Dar es Salaam Tanzania.

"Fursa hizo ni pamoja na kutangaza biashara, kutengeneza mtandao wa biashara na kutoa huduma mbalimbali wakati wa onesho, ni matarajio ya serikali kuwa taasisi na makampuni mbalimbali mtajitokeza kwa wingi katika kufadhili shughuli mbalimbali ili kunufaika na fursa za kujitangaza kupitia onesho hili la S!TE," amesema Balozi Dkt. Chana