Ijumaa , 9th Mei , 2014

Kamishna msaidizi wa madini kanda ya Mashariki na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania imewataka watu wote wanaojishughulisha na utafutaji wa madini ikiwemo uchimbaji wa kokoto na mchanga kupata vibali ili kuepuka usumbufu.

Kokoto zikiwa tayari kusafirishwa kwa ajili ya shughuli za ujenzi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na mkurugenzi wa usaidizi katika biashara kutoka TMAA Bw. Bruno Mteta wakati TMAA ikieleza na kutoa ufafanuzi juu bei mpya za madini ya ujenzi kwa Dar es salaam na Pwani kuongeza makusanyo ya mrahaba.

Amesema kitendo cha kuchimba mchanga au kuchimba madini ni kinyume cha sheria iwapo hatakuwa na leseni hivyo ni vyema wale wote wanaojishughulisha na shughuli hizo kujitokeza na kupata leseni kabla serikali haijawachukulia hatua.