Jumanne , 25th Aug , 2015

Waandishi wa habari mkoani Mbeya wamekumbushwa kutoandika masuala ya kisiasa pekee wakati huu wa mchakato wa uchaguzi mkuu na badala yake wajikite zaidi kuandika habari za kijamii ambayo ndio msingi mkuu wa maendeleo ya nchi.

Makamu wa mwenyekiti wa Mbeya Press Club Modestus Nkulu akifunga mafunzo ya waandishi wa habari

Akizungumza na east africa radio mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya Modestus Nkulu amesema kuwa waandishi wanawajibu wa kuandika masuala ya kijamii ili kuibua mambo mbalimbali yanayowagusa watu wa kada ya chini

Nkulu amesema kuwa wakati wa kampeni waandishi wa habari wanapaswa kuchukua tahadhari ili kuhakikisha usalama wao endapo viashiria vya uvunjifu wa amani vitatokea sehemu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao

Pia amewataka kutokubali kununuliwa na vyama vya siasa kwa lengo la maslahi ya wagombea na badala yake waandika habari zao kwa usawa kwa kufuata miiko maadili na taaluma ya uandishi wa habari.