Ijumaa , 12th Feb , 2016

Mwanasiasa machachari nchini Afrika Kusini Julias Malema ametolewa nje ya bunge baada ya kushiriki kukataa hotuba ya Jacob Zuma kwamba hatakiwi kuhutubia taifa hilo kwa kuwa ana kashfa za matumizi mabaya ya madaraka.

Mvutano huo umetokea baada ya spika wa bunge la Afrika Kusini mama Baleka Mbete na wafuasi wa upinzani wengi wao kutoka chama cha Ecoomic Freedom Fighters EFF wakiongozwa na Malema kutoelewana walipotaka utaratibu kuzuia Rais asihutubie.

Baada ya Spika wa bunge hilo kuwataka wapinzani hao wamsikilize Rais waligoma ndipo Spika akaamuru kutolewa nje kwa wabunge hao.

Baada ya hapo Rais Zuma aliendelea na hotuba yake ambapo alisisitiza kwamba serikali yake imeendelea kubana matumizi kwa lengo la kuwakomboa wananchi wa nchi hiyo.

Aidha Rais Zuma anakumbwa na kashfa ya kutumia fedha za umma kukarabati nyumba yake ya kifahari jambo ambalo limezua mjadala mkubwa nchini humo kwa muda sasa.

Chanzo BBC