Jumatano , 15th Mar , 2023

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge, amewataka wale wote wenye vituo vya kufanyia watu massage na havijasajiliwa wala kuwa na leseni wajisalimishe mara moja, kwani kufanya hivyo wanaikosesha serikali mapato.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge

Mnyonge ameyasema hayo kufuatia operesheni iliyofanyika kimyakimya na kubaini uwepo wa nyumba nyingi zinazofanya huduma ya massage na matendo ya ngono zembe.

Meya Songoro amesema madangulo kwa Kinondoni pekee yamegundilika kuwa yapo 512.