
Akiongea leo Jijini Dar es salaam Jaji Nsekela amesema baada ya zoezi la urejeshaji fomu kukamilika wamefanya uchambuzi na kuchagua idadi hiyo ya viongozi ili kuthibitisha uhalisia wa mali hizo kulinganisha na tamko la rasilimali na madeni la viongozi na uhalali wa mali zao zilivyopatikana.
Amesema kuwa zoezi hilo nyeti litachukua muda wa mwezi mmoja abapo litaanza Juni 18 na kumalizika Julai 18 ambapo viongozi waliochaguliwa tayari wamekwishapewa taarifa ili kuweza kuwaepuka watu wenye nia ovu ambao wanaweza kutumia zoezi hilo kama njia ya kujipatia manufaa.
"Kama mnavyojua sisi tunazungumzia suala zima la Maadili kwamba kiongozi awe na Maadili na mimi kama kiongozi na mmoja wapo wa viongozi nikitoa tamko langu na nikitaka kuhakiki tunataka tujue zile mali nilizo nazo na uwezo wangu kuna uwiano gani hapo, hizo mali nimepata kihalali au sijapata kihalali" amesema
Ameongeza kwamba "Sisi viongozi tunatakiwa tuwe na mali zilizopatikana kihalali na sio vinginevyo kwahiyo ndiyo zoezi kubwa tunaloenda kulifanya kuanzia tarehe 18 mwezi huu ndio tutaanza zoezi hilo la kuhakiki hao viongozi tuliowachagua na litatuchukua wiki nne au mwezi mmoja nadhani mpaka tarehe 18 mwezi July na kwasababu ni zoezi nyeti, tumeona ni vizuri viongozi kwanza tuwaambie kwamba kuna zoezi hilo linakuja”.
Hata hivyo amesema sababu ya kuanza na viongozi hao baadhi limechangiwa n sababu mbalimbali ikiwepo kutokuwepo na rasilimimali fedha za kutosha.
Disemba 27, 2017 Nsekela aliwahimiza Viongozi wa Umma kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu za tamko la rasilimali na madeni kabla ya Disemba 31 mwaka huo ambapo viongozi waliotakiwa kurudisha fomu waltakiwa kuwa 16339.