Jumanne , 21st Jun , 2016

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Selemani Jaffo amesema serikali inaendelea na mchakato wa kuajiri wanafunzi ambao wanamaliza katika vyuo mbalimbali vya afya hapa nchini.

Jaffo ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sumve Richard Ndassa CCM aliyetaka kujua mkakakati wa serikali katika kutatua matatizo ya huduma za afya hasa wahudumu baada ya wananchi kwa kushirikiana na serikali kujenga majengo.

Naibu Waziri Jaffo ameeleza kwamba serikali inatambua upungufu wa watumishi wa afya katika sekta ya afya hasa vijijini na kuahidi kwamba serikali itatengeneza mazingira mazuri ili watumishi wa afya wazeze kumudu kusaidia wananchi vijijini.

Aidha Naibu Waziri Jaffo amewapongeza wabunge kwa kupitisha bajeti ya serikali ya trilioni 29.5 na kuwaahidi wabunge kwamba mawaziri watajitahidi kwa kila hali kuhakikisha huduma na matumizi ya fedha kwenye miradi zinakwenda kwa wakati.