Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msimbati, alipokuwa katika ziara
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa maelezo ya utekelezaji wa REA, kwa mwaka wa fedha 2015/2016 na mpango wa utekelezaji wa bajeti hiyo.
Dkt. Kalemani amesema serikali imejikita katika kusambaza umeme mijini na vijijini ili kutimiza lengo lake la kuhakikisha kuwa asilimia 85 ya wananchi wanapata umeme ifikapo mwaka 2025.
Aidha, Dkt. Kelemani alieza kuwa kampuni zinazosambaza umeme vijijini zenye tuhuma mbalimbali ikiwemo za kufunga vifaa vya umeme chini ya kiwango, rushwa, kutolipa vibarua wakandarasi zitachukuliwa hatua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dkt. Lutengano Mwakahesya, amesema mradi wa REA awamu ya pili ulilenga kupeleka umeme katika makao makuu ya wilaya 13 nchini.