Jumanne , 2nd Apr , 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana kuacha kutumia dawa za kulevya hususani bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi iitwayo Cha Arusha na Skanka akisema aina hii ya bangi huwafanya wawe Vichaa na itawapoteza kwenye muelekeo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kilimanjaro leo April 02, 2024 Waziri Mkuu Majaliwa amesema dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi zimeendelea kutumiwa kwa wingi hapa nchini.

"Hivi karibuni kumeibuka aina nyingine ya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi inayofahamika kama #ChaArusha pamoja na #Skanka aina hii ya bangi yenye sumu nyingi huchanganywa kwenye sigara lakini ukishaitumia Watumiaji wanabadilika na kuwa Vichaa”

“Ni wakati mzuri sasa vijana ambao mmekuwa mkitumia Cha Arusha na Skanka muache ili kunusuru maisha yenu, vijana mnahitajika katika Taifa hili, vijana ndio mtakaolijenga Taifa hili, Vijana ndio muelekeo wa Taifa hili Cha Arusha na Skanka zitawapoteza kwenye muelekeo na mtalifanya Taifa hili likakosa Watanzania” alisisitiza Waziri Mkuu