
Profesa Issa Shivji, mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambaye anamaliza muda wake. na atamkabidhi kiti hicho kwa Profesa Penina Mlama.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Penina Mlama ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere litakalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia kesho.
Profesa Mlama amesema kuna haja ya vijana kuacha fikra potofu kuwa maendeleo yanaletwa kwa kuwa na fedha na utajiri, na badala yake wawe na fikra chanya ambazo amesema zitawasaidia kuanzisha miradi ya kimaendeleo ambayo itakuwa suluhisho la matatizo yanayowakabili.
Kwa upande wake, mmoja wa vijana ambaye ni mshiriki wa Kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Bw. Gotaji Mgina amewataka vijana kushiriki makongamano yanayoendeshwa na Kigoda hicho, kwa kuwa ndio suluhisho na namna ya kubadili fikra za kimaamuzi.