Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Madeni Tanzania (TCDD) Hebron Mwakagenda
Kauli hiyo ameitoa hii leo katika kongamano maalum la vijanana Katiba lililoandaliwa na taasisi ya TYVA lililofanyika jijini Dar es Salaam.
"Kijana wa Kitanzania jipiganie kwa sababu ya idadi mliyonayo, yaani pigana, sasa tatizo linalojitokeza kwa vijana sasa hivi njia rahisi waliyogundua ni kuwa machawa, sasa tukileta uchawa kwenye Katiba hatutaipata, kwa sababu si utakuwa nyuma ya mwanasiasa unaganda kwenye nguo," amesema Mwakagenda.
Aidha kwa upande wake Wakili Cosmas amesema, "Vijana wa nchi hii wanakumbana na changamoto nyingi sana linapokuja suala la ushiriki kwa masuala ya kisiasa hasa kwenye suala la Katiba Mpya, sisi ndiyo nchi pekee ambapo vijana wote waliokaa hapa ambao hawana msingi wowote wa kisheria inayowapa haki ya kupaza sauti yao kwenye platform mbalimbali za kisiasa".