Jumatatu , 8th Aug , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka vijana nchini kuingia kwnye sekta ya kilimo kani serikali imejipanga kuwapatia mashamba yenye hati na kuwasaidia wapate mikopo yenye riba nafuu.

Rais Samia akihutubia kwenye maadhimisho ya Nanenane jijini Mbeya

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 8, 2022, jijini Mbeya wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Nanenane.

"Niwaambie vijana njooni kwenye sekta ya kilimo tumejipanga kuwapatia mashamba na yatakuwa na hati na zitatoka kwa majina ya vijana watakaokuja, pia tumejipanga kuwaunga na mabenki ili mpate mikopo kwa riba nafuu," amesema Rais Samia