
Basila Mwanukuzi na Seki Kasuga
Karibu wa Itikadi na Uenezi CCM- Humphrey Polepole
Katika zoezi hilo la kuchukua fomu vijana wengi wa CCM wameonekana kuchangamkia nafasi hiyo ya ubunge wa EALA akiwemo aliyekuwa miss Tanzania wa zamani Basila Mwanukuzi, kada mkereketwa Seki Boniventure Kasuga na wengine wengi.
Huu ni mchakato wa ndani wa chama hicho ili kupata wawakilishi na Ndugu Humphrey Polepole amesisitiza uadilifu.
"Tumesisitiza tena rushwa na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na kanuni za uchaguzi na uongozi havitavumiliwa, wote watakaoshiriki matendo hayo vikao vya chama vitayaondoa majina yao". Alisema Polepole
Seki Kasuga
Chama cha CCM kinatakiwa kutoa wawakilishi 6 watakaokwenda kuwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika (EALA)
Basilisa Mwanukuzi akiwa ametoka kuchukua fomu