Jumatano , 29th Nov , 2023

Watu 13 wamefariki dunia na wengine 36 wakijeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ally's Star lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga treni ya mizigo katika makutano ya barabara na reli maeneo ya Manyoni mkoani Singida.

Ajali ya basi na Treni

Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dkt. Furaha, amethibitisha taarifa hizo na kwamba majeruhi wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika Hospitali za Itigi Mission na Hospitali ya wilaya ya Manyoni.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Novemba 29, 2023.