Moja ya nyumba zilijengwa kwa ajili ya kuwakopesha wananchi kwa gharama nafuu.
Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi mtendaji wa kampuni inayoshughulikia mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortagage Refinancing TMRC, Oscar Mgaya amesema mpaka sasa imetoa mikopo ya thamani ya sh. Bilioni 34.1 kwa benki wanachama.
Mgaya ameongeza kuwa licha ya changamoto hizo suala la mikopo ya nyumba lililoanzishwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya fedha,Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Benki kuu, kwa ushirikiano na benki za biashara na kwa ufadhili wa benki kuu ya dunia na kupiga hatua kutoka benki tatu hadi 20.
Aidha amesema kuwa kuongezeka kwa ushindani pia kumesaidia riba kupungua kutoka wastani wa zaidi ya asilimia 20 hadi wastani wa asilimia 18,takwimu kutoka benki kuu zikionyesha soko la mikopo ya nyumba kukua kwa asilimia 59 mwaka 2014.