Jumatano , 16th Mar , 2016

Uzinduzi wa Daraja la Kigambo uliokuwa ufanyike leo umesogezwa mbele kwa mara nyingine tena hadi tarehe 16 mwezi wa nne mwaka huu baada ya baadhi ya mambo kutokuwa tayari kwa matumizi ya Daraja hilo.

Muonekano wa Daraja la Kigamboni

Akiongea jana na Waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara katika daraja hilo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa amesema kuwa licha ya daraja hilo kuwa ukikongoni kukamilika lakini serikali inahitaji kujiridhisha zaidi kabla ya kuanza kutumika.

Prof. Mbarawa amesema kuwa kuna majarabio ambayo yanatakiwa kufanyika katika daraja hilo ikiwemo kujaribu kupitisha mizigo ya aina zote kwa kuwa daraja hilo litatumika kama kiungo muhimu cha usafirishaji mizigo ya aina yote.

Kwa upande wake Meneja ujenzi wa Daraja hilo Karim Mtaka, amesema kuwa daraja hilo bado linafanyiwa majaribio lakini pia wapo kwenye hatua za mwisho kutoa vyuma vilivyotumika kushikilia daraja hilo wakati wa Ujenzi