Jumatatu , 17th Aug , 2015

Kikao cha baraza kuu UVCCM kilichofanyika katika ukumbi wa mwalimu J. Nyerere Dar es saalam chini ya mwenyekiti wake Sadifa J. Khamis kimemuengua na kumfukuza Kamanda wao wa taifa ndugu Kingunge Ngombale Mwiru.

Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza na Waandishi wa Habari

Maamuzi hayo yamekuja baada ya baraza kuu kujadili na kutathimini mwenendo wa kamanda huyo hasa kipindi hichi cha mapambano.

Sadifa amesema kuwa wamedhamiria kufanya hivyo baada ya kubaini Kigunge anaonekana kuwa na mapenzi zaidi ya watu kuliko chama hivyo ni bora waachane na mzee huyo ili wazidi kusonga mbele.

Kikao hicho cha baraza kimefikia maamuzi hayo baada ya kuamini kuwa kamanda huyo kwa sasa hataweza kuivusha jumuiya hiyo katika kupata ushindi wa kishindo Oktoba 2015.