Jumatano , 4th Oct , 2023

Katibu Mkuu wa UVCCM Fakii Raphael Lulandala (MNEC) amesema umoja huo unalo jukumu la kukilinda Chama cha Mapinduzi na viongozi wake kwa wivu mkubwa bila kuogopa mtu yoyote.

Katibu Mkuu wa UVCCM Fakii Raphael Lulandala

Ameyasema hayo wakati anahutubia wananchi mkoani Dodoma mara baada ya mapokezi yake yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya UVCCM Dodoma leo Oktoba 4, 2023.

"Kutakuwa hakuna sababu ya kuwa na Katibu wa UVCCM kwenye wilaya zetu, kata zetu na mikoa kama Chama cha Mapinduzi kinashambuliwa katika maeneo yao, ukiona mchungaji wa kondoo amepigwa lengo sio mchungaji ni kondoo" amesema Lulandala.

Aidha amesema katika kupambana na hoja za wapotoshaji na walaghai ni ajenda ya kudumu ya UVCCM.