Uteuzi wa maDC wagusa kila kada

Jumapili , 20th Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, aliwahi kunukuliwa kuwa katika kujenga nchi atateua watu kwa kujali uwezo wao katika kuisaidia nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

Kauli hii imejidhihirisha kwenye uteuzi wa Wakuu wa Wilaya ambapo amegusa makundi mbalimbali huku watu wanaojihusisha na masuala ya Kijamii pamoja na wanasiasa wakipata nafasi.

Kwa upande wa Jamii uteuzi umemgusa Basilla Mwanukuzi ambaye ni mshindi wa Miss Tanzania miaka ya nyuma na kwa muda mrefu amekuwa akishughulika na masuala ya ustawi wa wanawake huku kwasasa akiwa ni mwandaaji wa shindano la Miss Tanzania. Amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Tanga.

Wanasiasa chipukizi nao hawajaachwa nyuma ambapo wapo Mbunge wa zamani Halima Bulembo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza.

Aidha wapo pia mbunge wa zamani Peter Lijualikali, ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi.

Aliyewahi kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari pia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Mwanasiasa na Mwanasheria Albert Msando pia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.

Chini ni orodha kamili ya Wakuu wa Wilaya.