
Matank ya mafuta
Katika marekebisho hayo waombaji wa zabuni hizo kuanzia sasa wanashindanishwa kwa kigezo cha unafuu wa meli na gharama za kuingiza mafuta hayo nchini.
Meneja Mkuu wa Wakala hiyo Bw. Michael Mjinja amesema hayo wakati wa zoezi la zabuni ya kupata kampuni itakayopewa kandarasi ya kuingiza mafuta yatakayouzwa na kutumia nchini kuanzia Novemba mwaka huu, na kwamba kigezo kikuu wanachokiangalia kuwa ni kampuni yenye kiwango cha chini cha gharama za kuingiza mafuta nchini.
Kwa mujibu wa Bw. Mjinja, sambamba na mabadiliko hayo, kunzia mwakani hakuna kampuni ya kigeni itakayoruhusiwa kushindania zabuni za uagizaji mafuta na kwamba kampuni zitakazoruhusiwa ni zile tu zilizosajiliwa na kutambulika na mamlaka za hapa nchini.