Jumapili , 18th Jul , 2021

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Mkurugenzi Mkuu wa Mkuki na Nyota Dkt Walter Bugoya wametoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula

Wameyasema hayo wakati wa wakikabidhiana juzuu ya vitabu vinavyoelezea historia ya SADC ambapo bei kubwa ya vitabu pamoja na lugha ya uandishi  inayotumika imetajwa kuwa ni sababu isiyowavutia Watanzania kuwa na mwamko wa kununua na kusoma vitabu licha ya mwamko wa Viongozi na watu wengine mashuhuri wa kuandika vitabu vya historia.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC ilianzisha mradi wa kuandika na kuchapisha historia ya Jumuiya hiyo ili kuwafanya wananchi wan chi wanachama kufahamu historia ya Jumuiya hiyo.