
Moja ya wahusika katika kesi hiyo ya mauaji ambaye ni mmiliki wa shule hiyo.
Akiwasilisha ombi la kusitisha kazi hiyo, mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, wakili Elikunda Kipoko amebainisha umuhimu wa wateja wake kuwepo, ukizingatia baadhi yao wameshakata rufaa.
Ikumbukwe kuwa wakati hukumu ya kesi hiyo ikitolewa siku ya Juni 3, 2019, Jaji wa Mahakama Kuu Firmin Matogolo, aliagiza vielelezo likiwemo panga lililotumika katika mauaji, na nguo za marehemu kuteketezwa, na kuagiza vielelezo vingine kama vile simu, iliyotumika kuwasiliana usiku na kuitana eneo la tukio, Jaji aliamuru vitaifishwe na Serikali.
Juni 3, 2019 Mahakama hiyo ilimhukumu kunyongwa hadi kufa, aliyekuwa mlinzi wa shule hiyo, Hamis Chacha, huku mmiliki wa shule hiyo Edward Shayo pamoja na aliyekuwa mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa wakihukumiwa kifungo cha miaka minne jela, kwa kuficha ukweli wa mauaji ya mwanafunzi huyo.
Aidha Naibu msajili wa Mahakama hiyo, Frank Mahimbari, amesema kutokana na kuwa washtakiwa wote hawapo mahakamani, hivyo ataandika samansi ili waletwe mahakamani kushuhudia zoezi hilo.
Humphrey Makundi(16) aliuawa Novemba 6, 2017, na kisha mwili wake kutupwa katika mto Ghona, takribani mita zaidi ya 250 kutoka eneo la shule hiyo.