
Wakazi wa eno la Kipunguni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, wakiangalia mabaki ya helkopta mali ya Wizara ya Maliasili na Utalii, iliyoanguka katika eneo hilo na kuuwa watu wote wanne waliokuwa ndani yake hivi karubini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Charles Chacha amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa wiki ya usafiri wa anga ambapo amesema kuimarika kwa usalama kunatokana na usimamizi mzuri wa usalama wa anga unaofanywa na mamlaka hiyo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi mkuu huyo wa TCAA ameyataka makampuni ya ndege nchini kuhakikisha kuwa yanaheshimu ratiba za safari zao na kuachana na mtindo uliopo hivi sasa ambapo safari na ratiba za safari za ndege zimekuwa zikiahirishwa mara kwa mara na kuleta usumbufu kwa abiria.
Chacha amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikishusha heshima ya usafiri wa anga nchini na kuifanya Tanzania isihimili ushindani wa kibiashara na makampuni ya ndege kutoka nchi nyingine katika ukanda huu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa TCAA ameyataka mashirika ya ndege yanayofanya biashara zake hapa nchini kuiga namna wenzao katika nchi nyingine wanavyoheshimu muda na ratiba za safari za ndege, kiasi cha kufanya mashirika hayo mara zote yaongoze na kuwa mashirika bora na makubwa kibiashara.
Awali, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dkt Shaban Mwinjaka ameelezea kuridhishwa na kiwango cha uwekezaji kwenye sekta ya usafiri wa anga na kwamba serikali hivi sasa imeanza kuchukua hatua za kurekebisha shirika la ndege nchini ATCL ili ifikapo mwakani shirika hilo lianze kujiendesha vizuri kibiashara, wakati ambapo upanuzi wa sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere utakuwa umekamilika.