Upelelezi kesi ya Sabaya wakamilika

Ijumaa , 18th Jun , 2021

Upelelezi wa kesi moja ya unyang'anyi wa kutumia silaha kati ya kesi tano zinazomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, umekamilika na kwamba ameanza kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo.

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole na Sabaya, alipofikishwa mahakamani leo Juni 18, 2021

Hayo yamejiri leo Juni 18, 2021, Jijini Arusha wakati kesi yake pamoja na wenzake watano ilipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa ajili ya kutajwa tena kwa mara ya pili.

Sabaya na wenzake watafikishwa tena Mahakamani Julai 2, 2021.

Sabaya na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la uhujumu uchumi na walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 4 mwaka huu.