Jumatano , 7th Feb , 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limeahidi kuisaidia Tanzania kwenye masuala ya lishe ili kukabiliana na udumavu wa watoto ambao unaathari katika ukuaji wa ubongo na uchumi.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Elke Wisch

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Bi. Elke Wisch, jijini Dodoma.

Chande ameliomba Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF), kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika juhudi zake inazozifanya kuboresha maisha ya wananchi wake na kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Elke Wisch, alisema UNICEF inaahidi kuwekeza kwenye lishe ya Watoto ili kusaidia kuondoa udumavu kwa kuwa udumavu unaathari katika ukuaji wa ubongo wa mtoto na pia kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.