Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez amesema umoja huo umekuwa ukishiriki katika utaratibu wa uchaguzi nchini Tanzania hususan kupitia shirika lake la mpango wa maendeleo UNDP na mashirika yake mengine ikiwemo UN Women na la Sayansi, elimu na utamaduni, UNESCO.
Amesema ushirikiano huo umuwezesha mabadiliko ya sera na sheria ili kuhakikisha uharaka wa mabadiliko ya kidemokrasia unaendelezwa ili kufikia viwango vya kimataifa.
Alvaro ameongeza kuwa ni muhimu wakati wa kuelekea kampeni na siku ya uchaguzi na hatimaye matangazo ya matokeo ya uchaguzi kuwe na mazingira ya amani, na kwamba umma uangalie utaratibu wa uchaguzi na matokeo ya uchaguzi kama ya haki na wazi na kama kiashiria kamili cha matakwa ya watu.