Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya
Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi kutoka Jumuiya ya ulaya Emilio Rossetti, amebainisha kuwa nchi za Umoja wa Ulaya zitaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali yenye tija kijamii na kiuchumi.
Naye Balozi wa Hispania nchini Tanzania Jorge Moragas, amesisitiza kuwa kwa nafasi yao wataendelea kuwasaidia vijana hasa kupitia kazi zao kiutamaduni sambamba na kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye kazi za sanaa na utamaduni.
Euro elfu 60 zilitolewa kama ruzuku kutoka umoja huo na kutarajia kutumia kuwawezesha vijana kufanya sanaa kwa njia za kisasa, huku baadhi ya vijana watakaonufaika na mradi huo wa Umoja wakishukuru sana kwa mradi huo kufanyika nchini Tanzania.



