
Machafuko hayo yalisababisha mapinduzi ya kijeshi kutoka kwa wanajeshi waliowahi kumweka Rajoelina madarakani kama kiongozi wa mpito katika nchi yake hiyo ya Bahari ya Hindi akiwa na umri wa miaka 34 pekee mwaka 2009.
Siku ya Jumanne, kitengo kile kile cha kijeshi kilichosaidia kuinuka kwa Rajoelina kilitangaza kuchukua madaraka nchini Madagascar na kumuondoa madarakani kama rais kufuatia wiki kadhaa za maandamano yaliyoongozwa na vijana mara hii dhidi ya Rajoelina na serikali yake.
Takriban asilimia 75 ya watu milioni 30 nchini humo wameathiriwa na umaskini, kwa mujibu wa Benki ya Dunia, kutokana na ukosefu wa elimu ya juu, ufisadi wa serikali na gharama ya maisha miongoni mwa masuala yaliyotawala maandamano ya hivi majuzi.
Wakati huo huo, Kanali Michael Randrianirina aliyeichukua nchi hiyo kijeshi ataapishwa kama rais wa Madagascar tarehe 17 Oktoba, katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii na kituo cha televisheni cha serikali.
Umoja huo hapo awali ulizisimamisha nchi kadhaa wanachama baada ya mapinduzi ya kijeshi, zikiwemo Mali, Burkina Faso na Guinea.