Jumatatu , 18th Jul , 2016

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema maafisa wa polisi ambao wamepandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wana kazi kubwa ya kuonyesha uwezo kwa aliyewateua.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba

Waziri Mwiguku ameyasema hayo wakati wa kuapishwa kwa maafisa wa jeshi la polisi leo Ikulu Jijini Dar es salaam.

''Ukiteuliwa una kazi ya ziada ya kuhakikisha unaonyesha kwamba unaweza tofauti na ambaye hakuteuliwa kabisa'' Amesema Waziri Mwigulu.

Aidha Waziri amemshiukuru Rais kwa mojo wake wa upendo kwa kuwapandisha vyeo maafisa hao kwani hakuna sheria ambayo inamlazimisha kufanya hivyo.

Jumla ya maofisa waliopandishwa vyeo ni maafisa 25 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP). Na 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ambapo wawili hawakuweza kufika kwa kuwa mafunzoni nje ya nchi.