hivyo itasaidia kuchagiza utawala bora kwa wananchi wa jimbo la Kibakwe kwa ujumla.
Ametoa kauli hiyo leo katika Kijiji cha Kinusi kilichopo Kata ya Ipera, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijni Dodoma wakati wa tukio la kukakabidhi eneo hilo la ujenzi wa Mahakama kwa mkandarasi.
Amesema mradi huo wa ujenzi wa Mahakama utakaogharimu shilingi bilioni 1.1 hadi kukamilika kwake umekuja kwa wakati muafaka kwani wananchi hawatalazimika kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kwenda kutafuta haki zao wilayani Mpwapwa.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa ujenzi wa jengo hilo unarudisha historia ya eneo hilo la Ipera kwani miaka ya 1952 kulijengwa Mahakama na Waingereza iliyoanza kufanya kazi huku aliyekuwa Chifu wa eneo hilo, Chifu Zaina Sechamule alitumika kama Hakimu.
"Kihistoria eneo hilo linajulikana kwa jina la Kwilondoo ndiko eneo ambako kulikuwa kunapatikana haki na ndilo eneo alikokuwa akiishi Chifu na huyu alikuwa ni Chifu mwanamke, hivyo leo ni siku ya kihistoria ya kukabidhi eneo la ujenzi wa mahakama ya kisasa," amesisitiza Waziri Simbachawene.
Amesema ujio wa mahakama hiyo itasaidia kutoa haki kwa zaidi ya wananchi wa Kata sita zilizopo katika eneo hilo huku akizitaja hata zile Kata za jirani za Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro zitanufaika pia.