Alhamisi , 24th Sep , 2020

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Amani Buza Omari Katoto amesema matukio ya uhalifu katika mtaa huo yamepungua tofauti na miezi miwili iliyopita.

Wananchi wa Buza wakisikiliza viongozi wao hawapo pichani

Akizungumza na EATV leo Katoto amesema kupungua kwa matukio hayo kumechangiwa na jitihada za wananchi za kusimamia masuala ya ulinzi shirikishi kwa kusaidiana na jeshi la polisi

Amesema matukio makubwa yaliyokuwepo miezi miwili iliyopita ni wananchi kuporwa mali zao kuvunjiwa nyumba na kuibiwa huku wengine wakikabwa hata nyakati za mchana.

"Kwa kweli kwa sasa nashukuru Mungu haya matukio yamepungua na watu wanaishi kwa usalama ni matumaini ulinzi utaendeleo kuongezwa na wahusika kuchukuliwa hatua "amesema Katoto