
Akiongea na East Africa Radio jijini Dar es Salaam, kuusiana na maendeleo ya maabara katika Manispaa ya Kinondoni, Msemaji wa Manispaa hiyo Bw. Sebastian Myowera amesema changamoto kubwa ni jinsi ya kuwa na wataalam wa kuendesha maabara hizo.
Bw. Myowera amesema, imekuwa ngumu kwa waalimu wa kawaida kutumia maabara hizo kwakutokuwa na ujuzi jambo ambalo linahitaji hatua za haraka ili kufanikisha azma ya kuwa na mafanikio kwenye elimu kwa vitendo.
Aidha, Bw. Myowera amesema Manispaa ya Kinondoni imekamilisha ujenzi wa maabra zake kwa asilimia kubwa hivyo ni vyema serikali kuu ikaangalia jinsi itakavyo wezesha shule za Sekondari kuwa na wataalam wa maabara.