Jumatano , 10th Feb , 2016

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto nchini Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu amesema hatua ya kuwapima wanafunzi kama wanatumia madawa ya kulevya

wangali mashuleni itawasaidia kuondokana na janga la matumizi ya dawa za kulevya nchini Tanzania.

Akizungumza katika makabidhiano ya gari la huduma ya dharura (AMBULANCE) kwa Kituo cha Uratibu wa Matukio ya Sumu nchin Kutoka Serikali ya Japan Waziri Ummy Mwalimu amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana kutumia dawa za kulevya kuwapima mapema kubaini endapo wanatumia ama la itasaidia kuondokana na janga la matumizi ya dawa za kulevya nchini Tanzania.

Mwalimu ameongeza kuwa kufuatia kutambulika kwa maabara ya mkemia mkuu kimataifa na kupewa ithibati maabara hiyo itumike kutatua changamoto za upimaji wa athari za kemikali nchini huku akiwataka watendaji kuongeza kiwango cha uadilifu ili kupata matokeo sahihi ya sampuli wanazozipima .

Kwa upande wake mkemia mkuu wa serikali Prof. Samuel Manyele amesema wanatambua umuhimu mkubwa walionao katika kuwahudumia watanzanzia ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana kwa vielelezo baada ya kupelekewa sampuli mbalimbali.

Mara baada ya kukabidhi gari la huduma ya dharura (AMBULANCE) kwa Kituo cha Uratibu wa Matukio ya Sumu nchini Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba amesema Serikali ya Japan imekuwa na mchango mkubwa kwa nchi nyingi za Afrika.