
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo mjini Moshi, wakati wa Kongamano la kumpongeza Rais Magufuli lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT, ambapo aliwakilishwa na Naibu Spika Ndugai.
Akisoma risala ya Spika Ndugai "ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa,na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi, na kwa kazi kubwa aliyoifanya hatutaona rushwa kwenye chaguzi zijazo."
Aidha Naibu Spika amesema lingine ni kushughulikia tatizo sugu la rushwa ndani ya Serikali, na ndani ya CCM hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa rushwa ya uchaguzi katika chaguzi zijazo.