
Wanawake waliobakwa wamekosa huduma za dawa na ushauri ikiwemo wale waliobakwa na kundi la wanaume wengi kutokana na migogoro inayoendelea nchini humo.
Umoja wa mataifa umeripoti kwamba baadhi ya wanawake wamebakwa mpaka mara tano katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.
Mwenyekiti wa jopo la umoja wa mataifa wanaojadili yanayojiri nchini Sudan kwenye kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa jijini Newyork Bi.Yasmin Sooka amenukuliwa akisema kwamba “Hebu fikiria mwanamke mmoja anabakwa na kundi la wanaume wenye silaha, hebu fikiria kama ni wewe ama ni mtoto wako na tukio hilo linajirudia mara kwa mara’’
Baadhi ya wanawake hubakwa wakati wakienda kutafuta kuni huku wakitishiwa kifo endapo watatoa taarifa za matendo hayo.