Ijumaa , 17th Apr , 2015

Zoezi la uandikishaji katika daftarai la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa kielekroniki Biometric Voter Registration (BVR) limekamilika mkoani Njombe ambapo dalili za wazi zimeonesha kuwa idadi ya kubwa wananchi mkoni humo wameandikishwa.

Waziri Mkuu akifatilia Zoezi la Uandikishaji BVR baada ya kuzindua.

Kituo hiki metembelea katika vituo mbalimbali ndani ya kata mbili za mwisho kukamilisha zoezi hilo kwenye kata ya Njombe mjini halmashauri ya mji vikiwemo vya mitaa ya Mgendela Kwivaha na Idundilanga na kuona idadi ndogo ya watu waliosalia katika foleni na baadhi ya vituo kutowa kuta watu.

Zoezi hilo katika kituo cha Mgendela inaonesha kukamilika kwa kuwaandikisha watu wote waliotaka kujiandikisha kuwa kuwa mpaka kufikia majira ya saa saba mchana watu walikiwa wakiingia moja moja kila baada ya dakika 20 hadi nusu saa na kuwaacha waandikishaji kupata hata muda wa kuotea jua.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mgendela Kata ya Njombe Mjini, Obadia Choga mtaa ambao viongozi wengi wa serikali wamejiandikisha katika kituo hicho akiwemo na Spika wa Bunge la Tanzania Anna Makinda na Mbunge wa Njombe, mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba, na kamanda wa Polisi.

Amesema kuwa wananchi katika mtaa wake zoezi hilo limeenda vizuri licha ya wakati linaanza kuwa na watu wengi na kubaki hadi wati 100 kwa siku kutokana na kuwapo kwa mwamko wa watu katika uandikishwaji.

Amesema kuwa kufikia siku ya mwisho wananchi walikuwa wakijitokeza kwa uchache kukiashiria kuwa wananchi wote kujiandikisha na kuwa waandikishaji wakijitokeza mmoja ndani ya dakika 20 hadi nusu saa.

Choga amesema kuwa zoezi hilo kwa mtaa wake wamefanikiwa bila kukutana na watu wasio raia wa Tanzania ambao wamekuwa wakifika katika mtaa huo na kuishi wakiwa ni wateja wa viazi na kuwa waandikishaji walikuwa makini kwa kuangalia lafudhi ya mtu.

Amesema kuwa pia wamekutana na wanafunzi walio na umri ulio chini ya kiwango wanacho hitajika kuandikishwa ambao wengi wao walikuwa wa shule za msingi na kukataliwa kuandikishwa na kupewa elimu ya kujiandikisha itakapo fika mdawao wa kujiandikisha.

Amesema kuwa tume imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria watu wote watakao kutwa wakiwa wamejiandikisha mara mbili kwa kuwapa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu ama kulipa pesa isiyo pungua milioni 5.

Kwa upandewake msimamizi wa uandikishwaji halmashauri ya mji Njombe Swiga Sanke amesema kuwa kwa upande wa takwimu za watu walio andikishwa katika halmashauri yake zinatolewa na tume na hivyo hata tathimini haitatolewa.

Zoezi hilo licha ya kutangazwa kuwa siku ya Jana kuwa ndio ya mwisho Kituo hiki kimeshuhudia siku ya leo watu wakijitokeza kuulizia zoezi hilo na mwendelezo wake kwa lengo la kujiandikisha na vituo lilivyo shuhudia watu hao ni kituo cha Idundilanga na buguluni ambapo katika vituo hivyo mashine zimeondolewa tangu jusi siku ambayo ilikuwa ya kumaliza daftari hilo.