Jumanne , 13th Dec , 2016

Benki ya Barclays Tanzania imeeleza mafanikio ya kampeni yake ya 'Ready To Work' kupitia Tuzo za EATV zilizohitimishwa hivi karibuni, ambapo benki hiyo ilikuwa mmoja wa wadhamini.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Barclays Bank Tanzania Aron Luhanga

Benki hiyo imesema lengo la kampeni hiyo ni kuwajenga vijana hususani  wahitimu wa vyuo vikuu ili waweze kukabiliana na tatizo la ajira kupitia tuzo hizo kwa kuwa burudani ni kishwawishi kikubwa kwa vijana.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Barclays Bank Tanzania Aron Luhanga  amesema bado kuna changamoto kubwa kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu kuweza kujiuza katika soko la ajira kwa hiyo kupitia Tuzo za EATV wako tayari kuwaelimisha vijana ili waweze kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesema wakati kampeni ya Ready To Work ilipoanzishwa, kulikuwa na kusuasua lakini baada ya kuingia katika tuzo hizi, mwamko umekuwa ni mkubwa, ambapo hivi sasa wanapokea simu takriban 400 kwa siku za vijana wanaohitaji kujiunga na mpango huo.

Msikilize hapa:- 

 

 

Tags: