Alhamisi , 19th Mei , 2016

Serikali imewataka wananchi kuivumulia serikali katika utekelezaji wa sera ya elimu bure ili kuona maeneo mengine ambayo yataweza kuwasaidia wazazi kupunguza mzigo wa kuwasomesha watoto wao hasa baada ya changamoto nyingi kujitokeza.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Akiongea leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya Papo kwa Hapo, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amewataka wazazi kuendelea kuchangia baadhi ya maeneo ambapo wanaona kunauhitaji wa kufanya hivyo ili kuboresha na kuweka mazingira mazuri zaidi ya watoto kusoma.

Mhe. Majaliwa amesema baada ya kuanza kwa sera hiyo serikali imegundua kuwa watoto wengi wa Kitanzania walikuwa hawapelekwi shuleni, na kuibuka kwa watoto wengi kumesababisha changamoto nyingine ikiwemo uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea kuweka utaribu wake kwa ajili ya kuongeza madawati lakini pia miundombinu ya vyumba vya madarasa, ili waoto waliokosa sehemu wapate mahali pa kukaa chumba cha kupata taaluma yao.

Mhe. Majaliwa amesema serikali haiwakatazi kuchangia kwa wale wenye uwezo na wengine pia wafanye hivyo ili kutatua changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza wakati wa kuanza kwa zoezi hilo.

Sauti ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa