Mkurugenzi wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan
Hayo yamesemwa na mtendaji mkuu wa umoja wa klabu za waandishi nchini UTPC Abubakar Karsan leo jijini Dar es salaam wakati wa kuadhimisha miaka 3 ya kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi aliyeuawa wakati akiwa kazini mwaka 2012.
Kwa upande wa Rais wa UTPC amesema tunapomkumbuka Daudi Mwangosi ni lazima waandishi wa habari wafanye kazi katika hali na mazingira ya kutotishwa au kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari.
Mwangosi aliuawa tarehe 2 Septemba 2012 wakati akifanya kazi za uandishi wa hapa katika eneo la Nyororo mkoani Iringa na ameacha mke na watoto wanne huku nyumba aliyomwachia mke wake na watoto wake ikidhulumiwa na mmoja wa wanasiasa wa hapa nchini.

