
Ametaja kupungua kwa gharama za intaneti na kupiga simu kama moja ya mafanikio muhimu katika kujenga taifa lenye teknolojia jumuishi kwa wananchi wote.
Aidha, Rais Samia amesema hatua hizi zimewasaidia wananchi wengi hasa vijana na wajasiriamali kupata fursa mpya za kiuchumi kupitia mitandao.