
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Waziri Kindamba, amesema hayo leo muda mfupi baada ya kutoa huduma hiyo kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo ambapo wagonjwa, madaktari pamoja na watu wote wanaotembelea hospitali hiyo watakuwa wakipata bure huduma za intaneti huku TTCL ikitumia shilingi milioni kumi kutoa huduma hiyo kila mwezi.
Akizungumzia msaada waliopata kutoka TTCL, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohammed Janabi amesema shilingi milioni 120 zilizokuwa zitumike kulipia huduma za intaneti, hivi sasa zitatumika kutoa matibabu ya bure kwa mgonjwa mmoja kila mwezi.