Donald Trump, mgombea urais wa marekani kupitia Republican
Katika kongamano hilo, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Paul Ryan, alitoa wito kwa wajumbe kumuunga mkono Bw. Trump baada ya kutokea kwa mgawanyiko miongoni mwao wakati wa ufunguzi wa kongamano.
Wazungumzaji katika kongamano hilo siku ya Jumanne walitumia muda mwingi kumshambulia Bi. Hillary Clinton anayetarajiwa kuteuliwa kuwania urais kupitia chama cha Democrats.
Gavana wa jimbo la New Jersey, Chris Christie, alimtuhumu Bi. Hillary kwa kutumia barua pepe yake binafsi kufanya mawasiliano ya kiofisi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na kwa kushindwa kusimamia vyema sera za nje kulikosababisha matatizo, katika nchi za Syria, Libya na maeneo mengine.





