
Akizungumza na waandishi wa habari katika kambi ya jeshi la anga ya Andrews mjini Washington, Trump alisema alizungumzia vita vya Ukraine na Putin, pamoja na hali ya Iran.
Alipouliza kama walikaribia kufikia makubalianao ya kusitisha vita Trump alijibu "Hapana, sikupiga hatua yoyote,"
Mazungumzo kati ya Marais kati ya Putin na Trump yalichukua karibu saa moja, alisema msaidizi wa rais wa Urusi Ushakov.
Katika mazungumzo hayo alizungumzia tena suala la kukomesha haraka iwezekanavya hatua za kijeshi, Ushakov alisema.
Kulingana na msaidizi wa Putin, mazungumzo kati ya viongozi hao wawili" yalikuwa ya wazi"
Mazungumzo ya mjini Istanbul yatasalia kuwa ya pande mbili kati ya Urusi na Ukraine, Ushakov aliongeza.
Kulingana naye, tarehe maalum ya duru ya tatu ya mazungumzo ya Istanbul, haijatolewa.
Putin alimwambia Trump kwamba Urusi haitalegeza msimamo wake wa kuondoa sababu za mzozo wa Ukraine, Ushakov alisema. Pia alisema kuwa suala la Marekani kuipatia silaha Ukraine lilijadiliwa.