Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Akiwasilisha mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano ya kuanzia mwaka mpya wa fedha 2016/2017 Bungeni Dodoma Jana Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa kuna ongezeko kubwa la fedha katika kugharamia mpango wa pili.
Dkt. Mpango amesema kuwa mpango wa pili wa Maendeleo umejielekeza katika maeneo makuu manne ambayo ni kukuza uchumi na kujenga msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo ya uchumi na maendeleo ya watu na kujenga mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji.
Dkt. Mpango amesema katika kukuza uchumi na kujenga uchumi wa viwanda amesema hatua wanazokusudia kuchukua kuongeza uzalishaji na tija katika sekta ya uzalishaji na sekta za Kilimo,Viwanda, Madini na Utalii.
Amesema baadhi ya vigezo vya uteuzi wa miradi ya kundi hilo ni uwepo wa fursa za kipekee za rasilimali za uzalishaji na masoko ya bidhaa na uwezo wa bidhaa hizo wa kuhimili ushindani wa kibiashara.