Jumatatu , 4th Mar , 2024

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kuhusu kudorora kwa utendaji kazi katika kuhudumia meli na shehena katika Bandari ya Dar es Salaam kulikohusishwa na mgomo wa wafanyakazi wenye madai mbalimbali ikiwemo kufutiwa mikataba yao ya kazi na

Bandari

kusema hakuna mgomo wala hujuma zozote bandarini hapo.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa TPA aliyesitishiwa mkataba wake kwa sababu zozote zile na kwamba hata menejimenti ya mamlaka hiyo inatimiza ipasavyo jukumu lake la kusimamia kikamilifu utendaji wa idara ya vitengo vyote vya operesheni za kibandari katika Bandari ya Dar es Salaam kwa saa 24 ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa weledi, kasi na ufanisi wa hali ya juu.

TPA imeongeza kuwa wote watakaobainika wanahusika na kusambaza taarifa za upotoshaji juu ya Bandari ya Dar es Salaam watachukuliwa hatua kali za kisheria.