Jumapili , 3rd Jul , 2016

Afisa Elimu chama cha Kutetea Abiria nchini Bw Gervas Rutaguzindwa ametaka kiwango kipya cha kodi kilichoanza kutozwa tarehe 01.07.2016 kiende sambamba na uboreshaji wa kituo hicho kwa kuwa kituo hicho kwa sasa hakina ubora wa kuwa kituo cha mabasi.

Afisa Elimu chama cha Kutetea Abiria nchini Bw Gervas Rutaguzindwa ametaka kiwango kipya cha kodi kilichoanza kutozwa tarehe 01.07.2016 kiende sambamba na uboreshaji wa kituo hicho kwa kuwa kituo hichocha Ubungo kwa sasa hakina ubora wa kuwa kituo cha mabasi cha Kimataifa kwa nchi za Afrika Mashariki.

Bw. Rutaguzindwa ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa Radio na kuongeza kuwa kutokana na mabadiliko hayo ya tozo ni wajibu wa serikali kuhakikisha mapato hayo yanaenda sambamba na kutengeneza miundombinu rafiki kwa watumiaji wa kituo hicho.

Amesema tozo hizo mpya kama zitabadilisha mazingira ya kituo hicho basi serikali kwa ujumla itaongeza pato la taifa.

Aidha, amesema sitofahamu inayoendelea kutokea ndani ya kituo hicho kwa sasa baina ya watumiaji ambao ni wasafiri na wenyeji wao na watoza ushuru kuhusu tozo mpya nikutokana na uongozi wa Jijini kuchelewa kutoa taarifa ya ongezeko hilo kwa muda mrefu hali ambayo taarifa hizo hazijawafikia watumiaji wengi wa kituo hicho.

Ameiomba serikali kuweka huduma muhimu ndani ya kituo hicho cha mabasi ya mikoani na yanayoenda nje ya nchi hasa zile za huduma za afya, mashine za kutoa pesa na huduma mbalimbali za kijamii.