Jumatano , 30th Nov , 2016

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba, amelitaka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kuongeza juhudi za mapambano kwa wavuvi haramu wanaotumia zana zilizopigwa marufuku na serikali.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba.

 

Waziri Tizeba amesema hayo Mkoani Mwanza wakati akizungumza na wadau wa uvuvi mkoani humo ambapo amegiza kupatiwa orodha ya maofisa wa polisi mkoani humo wanaodai posho ili kutekeleza msako dhidi ya wavuvi haramu.

Dkt. Tizeba ametoa kauli hiyo mara baada ya kufanya ziara katika viwanda vya kusindika minofu ya samaki pamoja na maeneo ya kuhifadhia samaki jijini humo ambapo alishuhudia samaki wadogo wasioruhisiwa kuviliwa wakiwa wanasindikwa kwenye baadhi ya viwanda.

Aidha Waziri huyo ameongeza kuwa kitendo cha baadhi ya wadau wa biashara ya samaki kuendelea kuinua samaki kutoka kwa wavuvi haramu ndiyo chanzo cha kuendelea kwa matukio hayo kutokana na bidhaa zao kupata soko kutoka kwa wafanyuabiashara hao.