Alhamisi , 9th Jun , 2016

Asasi za Kiraia Zinazosimamia Haki ya Kijinsia na Utetezi Kwa Wanawake Chini ya Mwamvuli wa Mtandao wa Kijinsia Nchini TGNP Zimetoa chapisho la tathmini ya Bajeti Kuu ya Serrikali Kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 Baada ya Bajeti Hiyo Kusomwa jana Bungeni

Katika Chapisho Hilo Lenye Kichwa Cha JE BAJETI HII NI YA VIWANDA AU WATU Asasi Hizo Zimehoji Masuala Kadhaa Ikiwemo vipaumbele vya bajeti hiyo pamoja na kuitaka Serikali Kuwajibika katika kusimamia kusanyaji wa mapato na kutafuta yyanzo mbadala yya mapato endelevu IlikKudhibiti kuendelea kukopa na kuongeza deni la taifa.

Chapisho hilo pia limepongeza hatua ya Serikali ya kuanzisha Mahakama Maalum ya Mafisadi ambayo huenda Ikawa chachu katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa humu nchini na uhujumu uchumi kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa Umma.

Nao baadhi ya wadau na wananchi kutoka asasi Hizo wamekosoa bajetih hiyo katika Sekta ya Afya ambayo wamedai Kuwa Bajeti hiyo haijazingatiakKumwezesha Mama Mjamzito kupata huduma Bora za Afya.